Wenger Awakebehi Mashabiki Wa Arsenal

Baada ya ushindi wa jana wa goli 2-1 dhidi ya Chelsea, Kocha wa Arsenal ‘Arsene Wenger’ amefunguka na kusema kuwa msimu huu ulikuwa ni msimu mbaya sana kwani aliandamwa na figisu figisu za baadhi ya mashabiki wakitaka ajiuzulu na kuwataka waende wakajitathmini kama sio kupima akili kwani mtu hawezi kuhukumiwa kwa kosa moja.


Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger akishangilia goli la pili jana usiku.
Kocha huyo raia wa Ufaransa amekuwa akikabiliwa na shutuma kali kutoka kwa mashabiki wa Klabu hiyo wakimtaka ajiuzulu katika klabu hiyo ambayo ameingoza tangu 1996.
Kuna baadhi ya watu wasioifahamu Arsenal walitaka nijiuzulu hilo sio tatizo ni upeo waoSijali ukosoaji kwa sababu tunafanya kazi ya umma, Ninaamini kuna tofauti kati ya kukosolewa na kuchukuliwa hali ambayo hairuhusiwi kwa mwanadamu”, alisema Wenger huku akiendelea kuwachana mashabiki wa Asenal


Tabia ya baadhi ya mashabiki msimu huu, ndio kitu kinachoniuma sana, Sio mtu wangu ambaye ameathiriwa lakini sura ya klabu hii duniani haipo hivyo, tabia hiyo haioneeshi tabia ya Arsenal, Nadhani kuna umuhimu wa baadhi yetu kupimwa akili kwanza “,Alisema Wenger kwenye mahojiano yake na Bein Sports.
Arsenal jana ilishinda goli 2-1 dhidi ya Chelsea kwenye fainali ya kombe la FA na kutwaa kombe hilo kwa mara 13 na kuwa klabu ya kwanza kuchukua Kmbe hilo kwa muda wote mbele ya Man United.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment