Ajira Mpya Za ualimu Zimeongozwa Kwa Wingi

SERIKALI itaajiri watumishi 52,436, kati ya ajira hizo sekta ya elimu itaongoza kwa kuajiri watumishi 16,516. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora), Angella Kairuki alisema bungeni jana kwamba watumishi hao wataajiriwa katika mwaka wa fedha 2017/18.
Alisema mgawanyo huo wa ajira utahusisha sekta ya afya itakayoajiri watumishi 14,102, Kilimo (1,487), Mifugo (1171), Uvuvi (320), Polisi (2,566), Magereza (750), Zimamoto (1177) na Uhamiaji (1,500), Hospitali za Mashirika ya kidini na hiari (174) na sekta nyingine zinazobaki zitaajiri watumishi 12,673.
Kairuki alitoa takwimu hizo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mpanda, Sebastian Kapufi (CCM) aliyetaka kujua Serikali ina mkakati gani kuajiri watumishi zaidi maeneo ya kipaumbele na yenye upungufu.
Kadhalika, Waziri Kairuki alijibu swali la msingi la Mbunge wa Busokelo, Fredy Mwakibete (CCM) aliyetaka kujua Serikali ina mpango gani wa kuajiri watumishi katika sekta mbalimbali ikiwamo ya walimu wa sanaa.
Katika jibu lake, Kairuki alisema utafiti uliofanywa na Ofisi ya Rais (Tamisemi) mwaka 2015/16 ulibaini kuwa ipo ziada ya walimu wa masomo ya sanaa 7,463 katika shule za sekondari.
“Serikali inaendelea kugawanya walimu hao kwa kuzingatia uwiano na mahitaji halisi ya walimu wa sanaa kwa kila mamlaka ya serikali za mitaa ili kila shule iwe na walimu wa masomo ya sanaa badala ya kuajiri walimu wapya,” alisema.
Hata hivyo, Serikali inaendelea kuajiri watumishi wa kada mbalimbali ambapo katika mwaka wa fedha wa 2016/17 watumishi 9,721 wa kada mbalimbali wamekwishaajiriwa kwa kuzingati

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment