Serikali imewaagiza viongozi wa serikali kuanzia ngazi za vijiji,kata hadi wilaya nchini kwa kushirikiana na jamii kwa ujumla kuwafichua Mangariba wanaoshirikiana na wazazi kuwawakeketa watoto wao hatua ambayo imekuwa ikiathiri afya za wasichana wakati wanapojifungua na kusababisha baadhi yao kupoteza maisha.

Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsi,wazee na watoto wakati akizungumza na mamia ya jamii ya katika kijiji cha Kiteluka kilichopo kata ya Msanja wilayani Kilindi wafugaji wakati wa sherehe za kitaifa za njia mbadala za uvushaji rika kwa jamii ya kabila la wamasai zilizohudhuriwa na wageni mbali mbali wa serikali kutoka ndani na nje ya nchi .
Aidha Naibu Waziri Kigwangalla amemwagiza Katibu mkuu wa wizara hiyo kuhakikisha utaratibu ulioundwa na shirika la AMREF Health Afrika,Tanzania wa njia mbadala za uvushaji rika zinafanyika nchini kote kwa kusambaza waraka maalum ili kuzuia tendo la ukeketaji ambalo limekuwa likidharaulisha jinsia ya kike.
Hata Mkurugenzi mkazi wa AMREF nchini Dkt,Filorence Temu amesema takwimu za kitaifa zinaonesha kuwa ni asilimia 10% ya wasichana ndio wanaokeketwa nchini kila mwaka lakini katika baadhi ya mikoa ikiwemo Manyara,Dodoma na Mara takwimu zao zinavuka hadi kufikia asilimia 30% hatua ambayo inaonekana kuwa tatizo hilo bado ni kubwa.Facebook