HABARI iliyotufikia hivi punde inaarifu kuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Felix Ngamlagosi (pichani).
Taarifa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu ambayo imesainiwa na Mkurugenzi wake, Gerson Msigwa inaeleza kuwa Ngalamgosi amesimamishwa kazi kuanzia leo Juni 11,2017’
Mwishoni mwa wiki inayomalizika leo Mamlaka hiyo ilitoa tangazo katika vyombo vya habari ilitoa taarifa kwa umma kwamba Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imepokea maombi ya kuongeza muda wa leseni ya kuzalisha umeme kutoka kwa kampuni ya uzalishaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) (“Mwombaji”).
Hivyo basi,EWURA ina uarifu umma na wadau mbalimbali kwa ujumla kuwasilisha maoni au pingamizi ili kufanikisha uchambuzi mzuri wa maombi haya.
Taarifa za ilitolewa chini ya kifungu cha 19 cha Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji, Sura ya 414 ya Sheria za Tanzania na kifungu cha 8 cha Sheria ya Umeme, Sura ya 131 ya Sheria za Tanzania.
Tayari wadadisi wa mambo wanahusisha kusimamishwa kazi huko kunatokana na tangazo hilo la kutafuta maoni ya wanachi ya kutaka kumuongezea mkataba IPTL.
Itakumbukwa kuwa Januari Mosi mwaka huu Rais Dk. John Magufuli, alitengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Felchesmi Mramba, katika hali inayoonesha kuwa Rais amekerwa na jaribio la Tanesco kupandisha bei ya umeme kuanzi.
Baada ya Mramba kutenguliwa nafasi yake alipewa Dk. Tito Esau Mwinuka kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO akimtoa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alikokuwa akifundisha.
Rais Magufuli, alichukua hatua hiyo siku mbili baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kuiidhinisha ongezeko la asilimia 8.5 ya ya bei ya huduma za umeme kwa kilichoelezwa kuwa lengo ni kukidhi gharama za uzalishaji wa umeme.
0 comments :
Post a Comment