Ndoa ni sehemu muhimu katika maisha ya mwanadamu. Kwa sababu inaweza kuwa chanzo cha amani maishani au chanzo cha simanzi na msongo wa mawazo.
Wataalamu wa masuala ya mahusiano, wanaeleza siri saba zitakazoifanya ndoa yako idumu na iwe yenye furaha siku zote.
- Msibadilishane
Wanasaikolojia wanasema, zile kasoro ndogondogo alizokuwa nazo mwenza wako kabla hamjaoana ndizo zilizokufanya uwe karibu naye kwa hiyo usizibadili. Wanasema wenza hudumu pale ambapo kila mmoja anatambua na kuzikubali tofauti za mwenzake.
2. Msifie
Mtaalamu wa mahusiano, John Gottman anasema wenza wenye furaha ni wale ambao hukubali kizuri alichonacho mwenzake na kumsifu. Siyo kumsifu kwa majirani bali kumwambia mwenzako uso kwa uso. Kama ni mzazi mzuri mwambie, au ana sauti nzuri, basi mwambie.
3. Jadilini ya nyuma kisha songa mbele
Wenza watadumu pale ambapo wataperuzi matukio mabaya yaliyowahi kutokea zamani kati yao kisha kujikita zaidi kwenye kumbukumbu nzuri zilizowahi kutokea kwako.
4.Msikilize
Ni changamoto lakini jitahidi kumsikiliza mwenza wako hata anaongea vitu vinavyokukera. Hili ni suala la muhimu katika mahusiano. Kingine cha muhimu, usimtetee mtu anayekinzana na mwenza wako.
5. Fanyeni kazi pamoja
Miongoni mwa vitu vitakavyomfanya mwenza wako ausikie uwepo wako, ni kufanya naye shughuli za nyumbani. Kuondoa malumbano ya nani anafua, kupika, kupeleka watoto shule fanyeni pamoja. Wataalamu wa mahusiano wanasema, kukaa pamoja mkifanya kazi kunaimarisha mahusiano.
6. Tatueni matatizo yenu pamoja
Hata kama kila mmoja ana changamoto zake, zijadilini pamoja hii ni salama zaidi hata kwa afya ya kimwili.
7. Tembeeni pamoja
Dk Greer, mtaalamu wa mahusiano anasema, wenza wanatakiwa kutembea pamoja (kwa miguu) angalau kwa dakika 30 kwa wiki. Wanasema ni njia bora ya kujua aliyonayo mwenza wako kuhusu kazi, maisha na inaondoa msongo wa mawazo.
0 comments :
Post a Comment