MBUNGE wa Jimbo la Hai na Kionozi wa Kambi rasmi Bungeni,Mh ,Freeman Mbowe ametunukiwa cheti cha heshima na jamii ya Waislamu katika wilaya ya Hai kutokana na jitihada zake zisizo na ukomo katika kuleta umoja katika Dini na Madhehebu mbalimbali.
“Tunaamini katka Uhuru wa kuabudu na kujieleza ,malumbano ya hoja na mijadala ,Kuvumiliana na kusamehe, Vitisho ,ugandamizaji na uonevu wa aina yoyote vinaweza kuendelea lakini havitaweza kushinda jamii yetu. Uhuru ni tunu ya sili tuliyopewa na Mwenyezi Mungu Mtukufu” yalieleza maeno yaliyopo katika Cheti hiycho.
“Tunaamini katka Uhuru wa kuabudu na kujieleza ,malumbano ya hoja na mijadala ,Kuvumiliana na kusamehe, Vitisho ,ugandamizaji na uonevu wa aina yoyote vinaweza kuendelea lakini havitaweza kushinda jamii yetu. Uhuru ni tunu ya sili tuliyopewa na Mwenyezi Mungu Mtukufu” yalieleza maeno yaliyopo katika Cheti hiycho.
Mh Mbowe alikabidhiwa cheti hicho na Mjumbe wa Baraza Kuu la Waisalmu (BAKWATA) Alhaji Habib Nasiwa , katika msikiti wa Lambo uliopo Machame wilayani muda mfupi baada ya kumalizika kwa hafla ya kushiriki futari iliyoandaliwa na mbunge huyo katika misikiti minne tofauti ya Modio ,Rundugai,Kibaoni na Lambo.
Cheti hicho kilichosainiwa na Sheakh Mkuu wa wilaya ya Hai,Sheakh ,Omary Mahmoud ambaye pia ni katibu wa msikiti wa Kibaboni Bomangombe kimetolewa ikiwa ni ni ishara ya kutambua mchango mkubwa unatolewa na Mbunge huo kwa Waislamu.
Akizinunguza mara baada ya kukabidi cheti hMjumbe wa Baraza kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Alhaji Habib Nasiwa alitoa shukrani kwa niaba ya waislamu wa jimbo la Hai kwa namna ambavyo ameendelea kujitoa pamoja na kuchangia ujenzi wa msikiti wa Lambo.
“Nimehemewa sana ,sidhani kama naweza kusema kiasi cha kutoshereza ,nimehemewa na kujaaa furaha ya kufikiwa na Mh Mbowe,halikua jambo rahisi la kumpata leo ,kwanza tukijua Bunge linaendelea kadharika tukijua kwamba ana majukumu mengine mengi lakini akaona ashiriki na sisi wilaya ya Hai.”alisema Nasiwa.
“Jambo fupi la kukushirikisha jioni ya leo,mheshimwa tunakupongeza kwa kujua umuhimu wa ramadhan kwa kuacha shughuli zako na kuja kushiriki nasi katika kutufuturisha,tunakupa asante sana na mungu akubariki sana,”aliongeza Alhaji Nasiwa.
Katika hafla hiyo ya kufuturisha ,Mh Mbwe alishiriki katika misikiti yote minne ambapokatika msikiti wa Mudio alitoa mifuko 100 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya msingi inayomilikiwa na msikiti huo na pia alikabidhi kiasi cha sh Mil moja kwa msikiti wa Rundugai kwa ajili ya mwalimu anayefundisha masomo ya dini katika shule ya Msingi na Sekondari za Rundugai
0 comments :
Post a Comment