Saudi. Polisi nchini Saudi Arabia, wamefanikiwa kuzuia shambulio la kigaidi lililopangwa ili kuushambulia msikiti Mkuu wa mji mtakatifu wa Mecca jana usiku.
Polisi hao, walirushiana risasi na watuhumiwa hao ambapo mmoja wao alijilipua ndani ya msikiti huo.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo Mansour al­Turki, amesema watu watano
akiwamo mwanamke wamekamatwa wakati wa operesheni ya kuwasaka wahalifu hao.
Maofisa watano wa polisi na watu wengine sita wamejeruhiwa, lakini hakuna vifo katika tukio
hilo.