Baba amchoma kisu binti yake baada ya kudai anataka kuolewa na muislamu


Mwanaume wa kikristu nchini Israeli anashutumiwa kwa kumchoma kisu na kumuua binti yake mara baada ya kutoridhishwa na hatua ya binti yake huyo kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume wa Kiislamu.
Mwendesha mshtaka wa kesi hiyo alisema kuwa, mwanaume huyo Sami Karra mwenye umri wa miaka 58 alimuua mwanaye nyumbani kwake Ramle, Israeli siku moja baada ya kuhitimu.
Shtaka linasema, mwishoni wa mwezi Mei binti huyo Henriette aliikimbia familia yake kutokana na vitisho na unyanyasaji wa wazazi wake, na kwenda kuishi na mama wa mpenzi wake kwa muda mfupi.
Pia shtaka hilo linaendelea kusema familia ya Henriette ilitumia vitisho dhidi ya binti huyo na mama wa mpenzi wake ili kumrudisha nyumbani.
Baada ya mashauriano ya pamoja ya watu wa ustawi wa jamii, Henriette aliamua kurudi nyumbani.
Hata hivyo baada ya siku kadhaa, Henriette aliiambia familia yake kuwa yuko tayari kubadili dini na kuwa muislamu.
Kwa mujibu wa mashtaka, baba yake Henriette alichukuwa kisu na kwenda kumchoma mwanaye huyo mara tatu na kuumua, mara baada ya kupata taarifa kutoka kwa familia yake.
Na hivi sasa Karra anashikiliwa na polisi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment