MAGUFULI ATOA MILIONI MOJA KUKARABATI DIRISHA ALILOHARIBU AKIWA SEKONDARI

Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli Akimuonyesha Mkewe Mama Janeth Magufuli kitanda alichokuwa akitumia kulala wakati akisoma kidato cha tatu katika shule ya seminari katoke iliyopo Biharamulo Mkoani Kagera,ambapo amemweleza mkewe kuwa alivunja hilo dirisha na mpaka leo halikutengenezwa ambapo leo hii amekabidhi kiasi cha shilingi milioni moja ili kukarabati dirisha na madirisha mengine ya shule hiyo, Mh Rais yupo mkoani Kagera kwa ziara ya siku mbili mkoani humo, 19 julai
Mapema leo asubuhi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ametembelea Shule ya Seminari ya Mtakatifu Karoli Lwanga Katoke alikosoma elimu ya sekondari ambapo ameendesha harambee iliyofanikisha kupatikana mifuko 1,000 ya saruji na mabati 150 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa majengo ya Seminari hiyo ambapo pia ametoa Shilingi Milioni 1 kwa ajili ya kutengeneza dirisha la bweni alilolivunja wakati akiwa kidato cha pili pamoja
na madirisha mengine yanayohitaji matengenezo.
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli Akimuonyesha Mkewe Mama Janeth Magufuli kitanda alichokuwa akitumia kulala wakati akisoma kidato cha tatu katika shule ya seminari katoke iliyopo Biharamulo Mkoani Kagera,ambapo amemweleza mkewe kuwa alivunja hilo dirisha na mpaka leo halikutengenezwa ambapo leo hii amekabidhi kiasi cha shilingi milioni moja ili kukarabati dirisha na madirisha mengine ya shule hiyo, Mh Rais yupo mkoani Kagera kwa ziara ya siku mbili mkoani humo, 19 julai
Dkt. Magufuli alienda shuleni hapo baada ya kuzungumza na wananchi wa Biharamulo Mkoani Kagera alipokwenda kufungua barabara ya lami ya Kagoma – Biharamulo – Lusahunga
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment