Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam PAUL MAKONDA amemwagiza Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es salaam kuwashusha vyeo maafisa elimu wa kata 12 baada ya maafisa hao kushindwa kueleza matumizi ya fedha za posho za madaraka kiasi cha shilingi laki mbili na nusu kila mwezi wanavyozitumia katika kutimiza wajibu wao.
MAKONDA ametoa maagizo hayo katika mkutano wake na Maafisa Elimu, Wakuu wa Shule za Msingi, Sekondari na Maafisa elimu wa Kata.
CHANZO TBC habari


0 comments :
Post a Comment