Taarifa ya Mahakama Kuu kuhusu maombi ya dhamana ya Yusuf Manji

Leo July 26, 2017 Mahakama Kuu ya Tanzania imesema inatarajia kuanza kusikiliza maombi ya dhamana yaliyotolewa na Mfanyabiashara maarufu Tanzania Yusuf Manji, August 4, 2017.
Jaji Isaya Arufani amesema hayo baada ya Mawakili wa Serikali Paul Kadushi na Simon Wankyo kuyapokea maombi hayo na kusema wana nia ya kuyapinga huku Jaji akisema anakubaliana na hoja zao na August 4, 2017 maombi hayo ya dhamana yataanza kusikilizwa.
Katika maombi hayo Yusuf Manji anaiomba Mahakama Kuu itengue hati ya kunyimwa dhamana iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa kuwa ana matatizo ya kiafya akisumbuliwa na matatizo ya moyo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment