Viongozi wa CHADEMA akijadiliana na Polisi mkoani Mwanza kabla ya kuanza kwa mkutano wa vijana
Chama cha Demokrasia na Mandeleo (CHADEMA) kimelaani hatua zinazochukuliwa na vyombo vya dola kukikandamiza ikiwemo kuwakamata na kuwashikilia na kuwahoji baadhi ya viongozi wa juu cha chama hicho akiwepo Katibu Mkuu Dkt. Vicent Mashinji na wabunge wawili waliokamatwa Jumamosi mkoani Ruvuma.
Kauli hizo zimetolewa jijini Mwanza na Naibu katibu mkuu wa chama hicho, Salum Mwalimu baada ya Polisi wa Wilaya ya Nyamagana kuvamia na kutaka kufunga kwa nguvu mkutano wao wa ndani uliolenga kuweka mkakati ya kukiimarisha chama chao.
Katika kongamano hilo la wanachama vijana wa CHADEMA wa Wilaya ya Nyamagana lilikutwa na kadhia hiyo baada ya Polisi kuvamia na kuwataka viongozi hao kusitisha mkutano huo kwa madai kuwa eneo hilo ni la wazi.
Lakini baada ya majadiliano kongamano hilo likapata baraka zote ambapo Naibu katibu mkuu CHADEMA, Salum Mwalimu licha ya kulaani kitendo cha kukamatwa kwa Katibu Mkuu wao Dkt. Vicent Mashinji na wabunge wawili wa chama hicho mkoani Ruvuma akawasihi wanachama kutumia changamoto hizo kama fursa ya kushika dola 2020.
Naibu katibu mkuu huyo pia pia akawatoa hofu vijana hao kuhusu baadhi ya wanachama na viongozi wa chama hicho wanaojiunga na CCM.
Hili ni kongamno la kwanza mkoani Mwanza tangu Serikali ipige marufuku mikutano ya hadhara ambapo wanachadema zaidi ya 500 wamekutana na kuweka mikakati ya pamoja ili kukijenga chama