Klabu ya Simba itasafiri siku ya Jumanne Alfajiri kulekekea Nchini Afrika Kusini kwa ajili ya Maandalizi ya Msimu Mpya wa 2017/18
Wachezaji waliopo Timu ya Taifa inayoshiriki maahindano ya CHAN wataungana na Timu mara baada ya Mechi ya Marudiano dhidi ya Rwanda Tar 22/07/2017
Ikiwa Afrika ya Kusini itacheza mechi za kujipima Nguvu na timu za kule ili Mwalimu aweze kuona Mapungufu na kuyafanyia kazi kabla ya Msimu kuanza.
Timu itarejea siku chache kabla ya Tamasha kubwa la kila Mwaka la Simba Day siku ya Tarehe 08/08/2017 ambapo kutakuwa na Mechi ya Kimataifa, aidha siku hiyo itatambulishwa Jezi Mpya pamoja na Kikosi kamili cha Msimu 2017/18


0 comments :
Post a Comment