Msafara wa Everton uliotua juzi jijini Dar es Salaam umewamwagia sifa na mashabiki pamoja na wapenzi wote waliojitokeza, wakisema ukarimu walioonyesha kwao ni faraja kubwa.
Taarifa waliyoandika kwenye mtandao wa klabu hiyo, ilieleza jinsi ambavyo walipata mapokezi makubwa siku ya kwanza walipowasili nchini.
Walishangazwa kuona watu wengi wakiwa wamevaa fulana za kuwakaribisha, jambo ambalo limewafurahisha kukutana na mashabiki wao jijini Dar es Salaam.



0 comments :
Post a Comment