IGP Sirro afanya mabadiliko kwa Makamanda wa jeshi la polisi

Amir jeshi mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimvua cheo cha Kamishna wa Polisi Simon Sirro na kumvalisha cheo cha Kamishna Generali wa Jeshi la polisi nchini Mei 29,2017 Ikulu jijini Dar es salaam
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Saimon Sirro, amefanya mabadiliko ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni pamoja na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga.
Katika mabadiliko hayo, aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Suzan Salome Kaganda amekuwa Mkuu wa kitengo cha Mafao na Fidia Makao Makuu ya Polisi, na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Murilo Jumanne Murilo ambaye alikuwa kamanda Polisi Mkoa wa Shinyanga.
Aidha, Nafasi ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga imechukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Simon Sylverius Haule, ambaye alikuwa Afisa Mnadhimu wa Polisi wa Mkoa wa Mara.
Uhamisho huo ni mabadiliko ya kawaida yanayotokea ndani ya Jeshi la Polisi katika kuongeza ufanisi wa utendaji kazi.
Imetolewa na:
Barnabus D. Mwakalukwa – ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment