Mnyika akunwa na kipaji cha Paul Clemen

t

Mbunge wa Jimbo la Kibamba jijini Dar es Salaam, John Mnyika ameshindwa kujizuia na kuonyesha mahaba yake hadharani baada ya kuguswa na kipaji cha mwanamuziki wa nyimbo za Injili, Paul Clement.
Hilo limetokea ikiwa ni siku mbili baada ya mbunge huyo kuhudhuria uzinduzi wa albam mpya ya muimbaji wa muziki wa injili, Baraka Mwaijande tukio lililofanyika Jumapili ya Julai 15, na kupambwa na wasanii mbalimbali wa muziki huo akiwemo Paul Clement.
Katika tukio hilo, Mnyika ambaye aliyekuwa mgeni rasmi, alijikuta akiinuka kwenye kiti chake na kujumuika na kijana huyo ‘stejini’.
Mbunge huyo ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, ametumia ukurasa wake wa twitter kummwagia misifa kijana huyo kwa kuandika “Nilibahatika kushiriki uzinduzi wa albamu za kijana Baraka Mwaijande, KKKT Temboni (Jimboni Kibamba). Nilifurahi sana. Nilifurahi na kuguswa na kipaji cha kijana Paul Clement; hasa wimbo wake “Amenyifanyia Amani!” Hakika amejaliwa kipaji”
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment