Jumanne July 11, 2017 Rais Magufuli amefanya uteuzi kwa kumteua Prof. Florens D.A.M Luoga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Prof. Florens D.A.M Luoga ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Taaluma) na anachukua nafasi ya Bw. Bernard Mchomvu ambaye Bodi yake ilivunjwa na uteuzi wake kutenguliwa.
Uteuziwa Prof. Florens D.A.M Luoga unaanza mara moja.