Askari wa usalama barabarani amefariki dunia baada ya kugongwa na gari aina ya Fusso asubuhi ya leo Jumatatu Julai 10, wakati akitekeleza majukumu yake huko barabara kuu inayotokea Tabora mjini kuelekea Wilaya ya Sikonge.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Tabora, SACP Wilbroad Mutafungwa, amethibitisha kutoke kwa tukio hilo na kumtaja askari aliyefariki kuwa ni E51 Koplo Aswile, ambaye alikuwa na wenzake wakifanya ukaguzi wa magari eneo la Itetemya Manispaa ya Tabora.
Akielezea tukio hilo, Kamanda Mutafungwa amesema kuwa askari hao walimuonyeshea ishara ya kusimama dereva wa gari hilo, Hassan Hussein na alitii kwa kupunguza mwendo kabla ya kuongeza mwendo ghafla, na kisha kumgonga askari huyo huku wengine wakikwepa dhahama hiyo kwa kurukia kando ya barabara.
Kamanda Mutafungwa amesema, gari hilo lilikuwa likitkea Sikonge na dereva wa lori hilo lenye namba za usajili T 564 ALG, alisimama hatua chache na kuamua kukimbia.
Kwa mujibu wa mwandishi wa Azam TV, Juma Kapipi aliyopo mkoani Tabora, amesema kuwa mara baada ya lori hilo kupelekwa kituo kikuu cha polisi cha mkoa huo, dereva huyo aliamua kujisalimisha kituoni hapo ambapo mpaka sasa yupo chini ya ulinzi.fusoFacebook