Kadinali na mweka hazina wa Kanisa Katoliki huko Vatican, George Pell, amerejea nchini Australia ili kujiandaa na utetezi wake dhidi ya madai ya unyanyasaji wa kingono.
Kardinali huyo mwenye miaka 76 na mshauri mkuu wa Papa Francis alionekana katika Uwanja wa Ndege wa Sydney jana alipowasili nchini humo ili kujibu shutuma zilizotolewa na jeshi la Polisi kuwa miaka ya 1970, Kardinali huyo aliwanyanyasa watoto kingono.
Hata hivyo, Pell amekuwa akikana shutuma hizo huku Julai 26 akitarajia kuwasili mahakamani kujibu shutuma zinazomkabili.
Kiongozi huyo alipewa likizo ili arudi nyumbani kupigania hadhi yake na inatajwa kuwa alipowasili Sydney hakusema lolote juu ya shutuma hizo zilizotolewa na watu mbalimbali waliodai kunyanyaswa kingono na Kardinali huyo.Facebook