Kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili wafanyabiashara James Rugemalira na Seth Habinder wa IPTL imeahirishwa hadi tarehe 22 mwezi huu.
Watuhumiwa hao walifikishwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo wakili wa serikali alisema upelelezi haujakamilika na hivyo kurudishwa mahabusu.
Aidha mawakili wanaomtetea mfanyabiashara Harbinder Singh Seth waliiomba mahakama imruhusu mteja wao akatibiwe nje ya nchi kwa madai kuwa ana uvimbe tumboni ambao umekuwa ukimsababishia maumivu makali na kumnyima usingizi kwa takriban wiki ya nne.
Hata hivyo ombi hilo limekataliwa mahakama na kuagiza kuwa mtuhumiwa huyo atibiwe katika hospitali ya Taifa Muhimbili.