Marekani imerudia kutoa wito wake kwa Serikali ya Congo DRC katika kuhakikisha wanafanya uchaguzi wa kihistoria na kukabidhi madaraka kwa amani.
Katika taarifa iliyotolewa na waziri wa nchi, Rex Tillerson, kwenye sherehe za miaka 57 ya Uhuru wa DRC , Marekani imesema, nchi hiyo iko katika hatua ambayo kura pekee na makabidhiano ya uongozi yanaweza kusaidia kurejesha kilichopotea kwa miaka mingi.
‘‘Nchi ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo iko njia panda katika kujenga fursa na kurejesha faraja muhimu iliyopotea kwa miaka mingi kupitia kukabidhiana madaraka kwa njia ya amani na demokrasia.
‘‘Tunawatakia kila la kheri Jamhuri ya Demokrasia ya Congo katika kufanikisha kile mnachokitamani kwaajili ya kujenga maisha bora ya baadaye kwa Wacongo wote, kwa kushiriki kwa uhuru Uchaguzi wa Kidemokrasia wa viongozi wao, na kunufaika kutokana na utajiri wa rasilimali za nchi yao, na kufanya kazi ya kujenga amani na mafanikio ya baadaye,’ ilisomeka taarifa hiyo.
Nchi ya DRC iliingia katika mzozo wa kisiasa mwaka uliopita baada ya kipindi cha utawala wa Rais Joseph Kabila kufikia mwisho, baada ya Mahakama ya nchi hiyo kumruhusu Kabila kuendelea kuongoza nchi hiyo.
Hata hivyo Umoja wa nchi za Afrika (AU) ilijaribu kutafuta suluhu ya kurejesha amani nchini humo lakini ilishindwa baada ya kanisa katoliki nchini humo kugomea mazungumzo ya upatanisho pamoja na vyama vya upinzani, chini ya mpango wa Desemba 31, 2016, ambao unamtaka Kabila kukabidhi madaraka baada ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.
0 comments :
Post a Comment