Uongozi wa Klabu ya Simba umesema kuwa Siku ya Simba maarufu kama ‘Simba Day’ ambayo huadhimishwa Agosti 8 ya kila mwaka, kwa mwaka huu itakuwa ni siku ya kihistoria ambayo itabaki kichwani mwa kila mwana Simba
Kaimu Makamu wa Rais wa klabu hiyo Iddi Kajuna ndiye aliyetoa taarifa hiyo wakati alipokutana na viongozi wa matawi kwa ajili ya kuzungumza kwa pamoja juu ya mustakabali wa uendeshwaji wa klabu, mipango ya ‘Simba Day’ na ushirikishwaji wa matawi pamoja na vyanzo vya mapato kwa klabu ya Simba.
Amesema wapenzi, mashabiki na wanachama wa Simba waisubiri kwa hamu siku hiyo, kwani pamoja na ‘surprise’ iliyoandaliwa kwa ajili yao, pia watapata nafasi ya kukishuhudia kikosi kipya kikicheza mchezo wake wa kwanza kabla ya kuanza kwa msimu ujao.
“Hatutarajii kucheza mechi ndogo, tunacheza mechi kubwa” amesema Idd
Mambo mengine ni kutambulishwa kwa jezi mpya itakayotumiwa na Simba msimu ujao pamoja na kuwafahamu wachezaji wote waliosajiliwa.
Kuhusu mchakato wa usajili, Kajuna amesema zoezi la usajili linaendelea kisayansi kwa kutegemea mapendekezo ya mwalimu na baada ya siku 10 taarifa rasmi itatolewa.
0 comments :
Post a Comment