Mfanyabiashara Said Ramadhani (22), mkazimwa Kimara Bucha amepandishwa kizimbani
katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni kwa kosa la kumbaka binti wa miaka 15 kinyume cha sheria.
katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni kwa kosa la kumbaka binti wa miaka 15 kinyume cha sheria.
Wakili wa Serikali, Daisy Makakala mbele ya Hakimu Joyce Mushi, amedai leo, Julai 24 kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Julai 6. Mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo.
Hakimu amesema dhamana kwa mshtakiwa ipo wazi akimtaka kuwa na wadhamini wawili ambao ni wafanyakazi kwenye taasisi inayotambuliwa na Serikali ambao watasaini bondi ya Sh1 milioni.
Mshtakiwa ameshindwa kutimiza masharti, hivyo hakimu ameamuru apelekwe mahabusu. Kesi itatajwa Agosti 7.
Wakati huohuo, wakazi wawili wa Ubungo Kibangu, Rashid Mrisho (45) na Aloyce Ludovick (30) wamepandishwa kizimbani mahakamani hapo kwa kosa la wizi wa mifugo.
Mwendesha mashtaka, Mussa Mansini amedai washtakiwa hao kati ya mwaka 2016 hadi Juni 2017 waliiba mifugo ya Mary Kapongo.
Wanadaiwa kuiba ng’ombe 18 wenye thamani ya Sh10 milioni na mbuzi 32 wenye thamani ya Sh2.5 milioni. Mbele ya Hakimu Issa Kasailo, washtakiwa wamekama mashtaka.
Hakimu amesema dhamana ipo wazi akiwataka kila mmoja kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh5 milioni.
Washtakiwa walishindwa kutekeleza masharti ya dhamana na wamepelekwa rumande hadi
Agosti 7 kesi itakapotajwa.
Agosti 7 kesi itakapotajwa.


0 comments :
Post a Comment