ANAYEKALIA KITI CHA MALINZI TFF AHOJIWA UHAMIAJI

Kaimu Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF, Wallace Karia leo mchana amehojiwa kwa zaidi ya saa moja na maafisa wa idara ya uhamiaji kitengo cha uraia juu ya uhalali wa uraia wake nchini.
Msemaji wa idara hiyo Ally Mtanda amekiambia kipindi cha Mshike Mshike viwanjani cha Azam TV kwa njia ya simu kwamba wamefikia uamuzi huo wa kumhoji kufuatia kupokea barua kutoka TFF ikitilia shaka uraia wake.
Mbali na kukaimu urais wa TFF tangu mwanzoni mwa mwezi huu, kufuatia Rais wake, Jamal Malinzi kuwekwa rumande kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha za shirikisho, Karia ni kati ya wagombea sita waliopitishwa kugombea urais wa TFF katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment