Kocha wa Manchester United Jose Mourinho, amesema upo uwezekano wa mshambuliaji wake Zlatan Ibrahimovic kuichezea tena klabu hiyo inayotumia dimba la Old Trafford.
Mashetani hao wekundu hawakumpatia mkataba mpya Ibrahimovic mwishoni mwa msimu uliopita, baada ya mchezaji huyo kusumbuliwa na jeraha la goti
Hata hivyo mpachika mabao huyo mahiri aliendelea kusalia klabuni hapo wakati akijiuguza, huku akitumia vifaa vya United vilivyopo uwanja wa mazoezi wa timu hiyo Carrington na hata wataalamamu wa tiba.
Kocha Mourinho hadhani kama Mswedeni huyo ambaye hakujiunga na wenzake waliopo Marekani kwaajili ya maandalizi ya msimu mpya, kuwa fiti mpaka kufikia mwezi Desemba.
Pamoja na yote hayo meneja huyo mwenye maneno mengi, ametanabaisha kuwa Kadabra anaweza kuendelea kuvaa uzi wa Manchester katika msimu ujao.
“Inawezekana, ipo wazi” alisema Mourinho. “Tulitaka kuwa waaminifu na kuwa wawazi na pia kufanya maamuzi, kama mapenzi yake yalikuwa kuondoka” aliongeza kocha huyo.
“Tuliacha nafasi ya muda kwa kila mmoja kuamua, na kutoka katika mtazamo wake, aliamua kwamba bado anaendelea kuhitaji kucheza katika kiwango cha juu” alisema Mourinho


0 comments :
Post a Comment