Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi, amelazimika kukesha ofisini kwake pamoja na wananchi takriban 189 wenye matatizo na kero za ardhi, usiku wa kuamkia leo Jumamosi Julai 15, jijini Dar es Salaam.
Lukuvi ametumia takriban saa 20, kusikiliza kero za wananchi ambao waligoma kuondoka ofisini kwake hadi shida zao zitakapopatiwa ufumbuzi.
Kazi hiyo ilianza majira ya saa 2 asubuhi hadi saa 9 usiku.
Hata hivyo wananchi hao walilazimika kulala wizarani hapo wakisubiri kuonana na waziri huyo, kutokana na idadi yao kuwa kubwa.
Wananachi wengi wenye matatizo na kero za ardhi ni kutoka maeneo ya Bagamoyo, Kibaha, Mkuranga, Kibiti na Dar es salaam.
Kwa ujumla wametumia fursa hiyo ya kipekee ya kuonana na kiongozi huyo wa wizara yenye dhamana ya ardhi na kumuelezea kero zao na hatimaye kupatiwa ufumbuzi papo hapo.
Wananchi hao wamesifu hatua hiyo ya Waziri Lukuvi kukutana nao ana kwa ana na kuzitatua kero zao za ardhi huku wakidai kuwa haijawahi kutokea kufanyika jambo kama hilo.Facebook