Mahakama nchini Sudan imemuhukumu mwandishi wa habari na mwanaharaka wa haki za binadamu, Amal Habani kulipa adhabu ya pauni za Sudan 10,000 sawa na Dola za kimarekani 1,499 au kutumikia kifungo cha miezi minne jela kwa kosa la kuwazuia afisa usalama kutekeleza majukumu yake.
Mwandishi huyo alikataa kulipa adhabu hiyo jana, Jumatatu na kuamua kwenda jela kutumikia adhabu yake licha ya kuwepo kwa jitihada za wanaharati wengine kutaka kulipa adhabu hiyo, amesema mume wa mwandishi huyo, Shawqi Abdel-Azim, wakati akizungumza na waandishi wa Sudan Tribune.
Waliomshtaki katika kesi hiyo ni afisa usalama wa Taasisi ya ulinzi na Usalama wa Taifa (NISS) ambaye amedai kuzuiwa kutimiza majukumu yake wakati wa kesi ya kundi la wanaharakati wa haki za binadamu mjini Khartoum mwaka jana, wameripoti Sudan Tribune.
Tangu awali Amal Habani amekuwa akisisitiza kukamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi na afisa usalama ambaye hakuwahi kujitambulisha na kumtuhumu kuwapiga picha wakati wa kesi hiyo.
“Afisa wa NISS alinipiga kibao cha uso, na baada ya kukaa chini ya ulinzi kwa saa mbili niliachiwa na kurejeshewa simu yangu.”alinukuliwa na moja ya tovuti nchini humo.
Waandishi nchini Sudan wamekuwa wakikabiliwa na vikwazo vingi nchini humo vikiwemo vya kukamatwa. Mwezi Februari mwaka jana, maafisa usalama walikamata mashine za kuchapisha magazeti 14 bila kutoa maelezo ya hatua yao hiyo.
Jana Jumatatu, NISS pia wamekamata nakala za magazeti mawili ya michezo yaliyochapisha habari za kinachoendelea kuhusu sakata la Shirikisho la Soka Sudan (SFA) baada ya uamuzi wa FIFA kuwafungia kushiriki michezo hiyo kimataifa.
Katika nyakati kadhaa, waandishi wa habari wasio na mipaka, wamekuwa wakituhumu tabia za shirika hilo la usalama wa Taifa.
NGO nazo pia zimepigia kelele mamlaka za nchini humo kujitathimini katika hatua zake za kukiuka uhuru wa kujieleza.
Nchi ya Sudan iko katika nafasi ya 174 kati ya 180 katika mujibu wa takwimu za mwaka 2017 za Uhuru wa vyombo vya Habari Duniani na kuiweka kuwa moja ya nchi yenye ukandamizaji wa habari wa