Msimu mpya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara mwaka 2017/18 unatarajiwa kuanza kutimua vumbi Agost 26 mwaka huu, huku watani wa jadi katika soka la Bongo Simba na Yanga wakikinukisha Oktoba 14, siku ambayo itakuwa ni ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
Ligi hiyo itakayorushwa mubashara kupitia Azam TV, inatarajiwa kuanza kwa mchezo wa ngao ya jamii utakaopigwa Agosti 23 katika dimba la taifa na utazikutanisha bingwa wa ligi kuu msimu uliopita Yanga, dhidi ya mabingwa wa Kombe la Shirikisho ambao ni Simba, na itahitimishwa Mei 20, 2018.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, mechi za ufunguzi Jumamosi ya tarehe 26 zitakuwa kama ifuatavyo:
Ndanda FC Vs Azam FC
Simba SC Vs Ruvu Shooting
Mwadui FC Vs Singida United
Mtibwa Sugar Vs Stand United
Kagera Sugar Vs Mbao FC
Njombe Mji Vs Tanzania Prisons
Mbeya City Vs Majimaji
Siku ya Jumapili mabingwa watetezi Yanga watakuwa nyumbani kuwakaribisha Lipuli FC ambao wamepanda daraja msimu huu wakiwa pamoja na Njombe Mji na Singida United.
Ligi ya msimu huu itazikosa timu za JKT Ruvu, African Lyon na Toto Africans ambazo zilishuka daraja msimu uliopita.Facebook