Hakimu aliyekuwa amepangiwa kusikiliza kesi ya Mbunge wa Arusha Godbless Lema Mh. Patrisia Kisinda amejitoa kuendelea kusikiliza shauri hilo baada ya wakili wa upande wa Jamuhuri Bi. Sabina Silayo kumtaka afanye hivyo kwa madai kuwa ni rafiki wa karibu na mke wa Mh.Godbles Lema.
Sambamba na hatua hiyo pia Mahakama ya wilaya ya Arusha imeendelea kushindwa kumsomea Mh. Lema maelezo ya awali ya kesi ya uchochezi dhidi ya Rais Mh. Dkt. John Magufuli inayomkabili, baada ya Mh. Lema kushindwa kufika Mahakamani kwa sababu zilizoelezwa na wakili wake Bwana. Sheki Mfinanga kuwa ni mgonjwa.
Akiwa Mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mh.Kisinda, wakili wa Lema Bw. Sheki Mfinanga aliwasilisha nakala ya hati ya matibabu inayoonyesha kuwa Mh. Lema ni mgonjwa na kuomba shauri hilo lipangiwe siku nyingine.
Baada ya Mh. Hakimu Kisinda kuyakubali maombi hayo ndipo wakili wa Jamuhuri Sabina Silayo akadai kuwa hata kama Mh. Lema angekuwepo wasikubali shauri hilo liendelee kwa kuwa hawana imani na hakimu Kisinda
kwani ni rafiki wa mke wa Lema huku akimuomba ajiondoe kwenye shauri hilo.
kwani ni rafiki wa mke wa Lema huku akimuomba ajiondoe kwenye shauri hilo.
Baada ya tuhuma hizo hakimu kisinda ambaye alisema yeye hana urafiki na mke wa Lema bali anamfahamu ,aliahirisha shauri hilo kwa muda na aliporejea ndipo akaeleza kuwa amekubali kujiondoa kwenye shauri hilo ili haki itendeke madai ambayo hata hivyo wakili wa Lema sheki mfinanga amesema hayatoshi kumfanya hakimu kujiondoa kwenye kesi.
Baada ya hayo Mh.Hakimu Kisinda akaahirisha kesi hiyo hadi tarehe 2/08/2017 ambapo sasa jalada la shauri hilo linatarajiwa kurudishwa kwa hakimu mfawidhi ili kupangiwa hakimu mwingine.
Huyu ni hakimu wa pili kujitoa kusikiliza kesi hiyo kwa sababu mbali mbali, hakimu wa kwanza kujitoa alikuwa Mh.Desideri Kamugisha ambaye alieleza kuwa alikuwa na kesi nyingine ya mtuhumiwa huyo huyo
hivyo hakuona ni busara kuwa na kesi mbili za mtu mmoja wakati kuna Mahakimu wengine.
hivyo hakuona ni busara kuwa na kesi mbili za mtu mmoja wakati kuna Mahakimu wengine.
Mh.Lema anadaiwa kuwa mnamo wa tarehe 22/10/2016 akiwa katika mkutano wa hadhara katika eneo la kambi
ya fisi jijini Arusha alitoa maneno ya uchochezi dhidi ya Rais Dkt. John Magufuli maneno ambayo pia
aliendelea kuyatoa siku iliyofuata tarehe 23/10/2016 pia akiwa katika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya shule ya sekondari baraa pia iliyoko jijini Arusha.

0 comments :
Post a Comment