Zaidi ya wafuasi 100 wa Serikali wamevamia Bunge la Venezuela na kuwapiga wabunge.
Mashuhuda wanasema kuwa wakati watu hao wanavamia bunge hilo lenye wabunge wengi wa Upinzani, vikosi vya usalama vilisalia kuwatazama tu bila kuchukua hatua.
Serikali imeahidi kufanya uchunguzi wa tukio hilo ambalo limejiri baada ya wabunge hao kuadhimisha uhuru wa nchi hiyo ndani ya Bunge.
Spika wa Bunge hilo, Julio Borges amesema kuwa zaidi ya watu 350, wakiwemo waandishi wa habari 108, wanafunzi na wageni wengine walizingirwa kwa saa kadhaa ndani ya jengo hilo.
Pia Spika huyo anasema wabunge watano wamejeruhiwa na wengine kupelekwa hospitalini kwa matibabu zaidi.
Venezuela kwa sasa iko katika mgogoro mkubwa wa kisiasa hali ambayo imesababisha nchi hiyo kutokuwa na utulivu huku uchumi wake ukiwa nyongefu.
Wapinzani wa nchi hiyo wanapinga mabadiliko ya katiba yaliyoitishwa na Rais Nicolás Maduro ambaye wanataka aondoke madarakani.
0 comments :
Post a Comment