Wapinzani Uganda wala ‘kibano’ kama wa Tanzania

Askari Polisi nchini Uganda wakiwa katika majukumu yao ya kawaida


POLISI nchini Uganda imewatia mbaroni wapinzani waliofanya mkusanyiko wa kupinga serikali wiki iliyopita, anaandika Hellen Sisya.
Emilian Kayima, Msemaji wa jeshi la polisi nchini humo amesema kuwa, karibu wapinzani 20 wa kundi moja la upinzani akiwemo kiongozi wa kundi hilo, walitiwa mbaroni siku ya jana kwa tuhuma za kufanya mkutano kinyume cha sheria.
Kayima ameongeza kuwa, watu wengine 56 walitiwa mbaroni siku ya Jumatano kwa kuhusika na tuhuma hiyo.
Wapinzani nchini humo wamekuwa wakifanya maandamano ya kupinga kile wanachosema kuwa ni njama za Rais Yoweri Museven wa taifa hilo za kutaka kubadili katiba kwa lengo la kubakia zaidi madarakani, ingawa yeye mwenyewe amekuwa akikanusha tuhuma hizo.
Alhamisi ya jana wapinzani walitia saini tambara la maoni katika kulalamikia mpango wa serikali wa kuifanyia mabadiliko katiba ya Uganda kwa lengo la kuondoa ukomo wa umri kwa rais wa nchi hiyo.
Katika katiba ya sasa kumeainishwa mpaka na umri wa miaka 75 kwa ajili ya urais. Kwa sasa Rais Yoweri Museven ana umri wa miaka 72 akiwa madarakani tangu mwaka 1986 na kwa mujibu wa katiba nchi hiyo Museven anatakiwa kuondoka madarakani ifikapo mwaka 2021.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment