Vyuo vikuu vya ‘wababaishaji’ kukiona


TUME ya vyuo vikuu nchini (TCU), imesema itachukua hatua kali za kisheria dhidi ya vyuo vikuu ambavyo vitatangaza kozi ambazo hazitambuliki na tume hiyo pamoja na Baraza la Taifa la Elimu ya ufundi (NACTE), anaandika Hellen Sisya.
Akizungumza na wanahabari, Eleuther Mwageni, Kaimu Mkurugenzi wa TCU amevitaka baadhi ya vyuo ambavyo tayari vimeonekana kutangaza kozi zisizotambulika na tume hiyo kuacha mara moja, kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.
“Wakiendelea kufanya hivyo, tunafata sheria zetu, tutachukua hatua stahiki ……..kuna adhabu zinatolewa,” amesema Mwageni.
Aidha, Kaimu Mkurugenzi huyo amewataka waombaji wa nafasi za masomo ya elimu ya juu nchini kuomba kozi ambazo zinatambulika na tume hiyo pamoja na NACTE na kuvisisitiza vyuo vikuu kote nchini kudahili wanafunzi wenye sifa na vigezo stahiki katika kila kozi.
Zoezi la uombaji wa vyuo kwa wanafunzi wanaotaka kujiunga na elimu ya juu hapa nchini linatarajia kuanza tarehe 22 Julai, mwaka huu ambapo wahitimu wa elimu ya kidato cha sita pamoja na wahitimu wa ngazi ya stashahada wenye sifa stahiki wataomba kudahiliwa na vyuo vikuu.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment