Bunge lafanya vioja, ripoti ya Lissu yayeyuka

TAARIFA iliyotarajiwa kuwasilishwa bungeni leo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi, Usalama na Mambo ya Nje, Adadi Rajabu kuhusu kushambuliwa kwa Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki imeota mbawa, anaandika Dany Tibason.
Taarifa hiyo ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu na wabunge pamoja na wananchi imeshindwa kuwasilishwa bungeni kutokana na mwenyekiti wa kamati hiyo kudai kuwa muda wa kamati hiyo kufanya kazi kwa ufasaha haukutosha.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Adadi Mohamed Rajabu ambaye ni Mbunge wa Muheza kwa kudai muda waliopewa kukamilisha ripoti hiyo ni mdogo hivyo hawakuwahi kukamilisha.
Kamati hiyo ya Ulinzi na Usalama ya Bunge inatarajiwa kukutana kuanzia kesho ili kujadili na kuiwasilisha ripoti hiyo katika bunge lijalo litakaloanza mwezi Novemba 2017.
Ikumbukwe kwamba baada ya kutokea tukio la kushambuliwa kwa risasi Tundu Lissu, Mbunge wa Nzega Mjini Hussein Bashe aliwasilisha hoja ya kulitaka bunge liunde kamati maalum ya kuchunguza tukio hilo ili iweze kubainika aliyefanya tukio hilo, na Spika Mhe. Job Ndugai alikubali na kupitisha hoja hiyo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment