Zinaweza
kuwa taarifa za kuwashtukiza mashabiki wengi wa Manchester City lakini
haina jinsi kuona kiungo mshambualiaji wa klabu hiyo, Kevin De Bruyne
akiwa nje ya dimba wakati timu yake ikipambana na Barcelona katika
mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Oktoba, 19 mwaka huu.
Jambo
hilo linakuja baada ya kutolewa taarifa ya De Bruyne alipata majeraha
ya misuli ya paja katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya Swansea hivyo
atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki nne.
De
Bruyne alitolewa katika dakika ya 81 ya mchezo huo ambao Man City
ilipata ushindi wa goli 3-1, na kwenda kufanyiwa vipimo ambavyo
vimeonyesha kuwa alipata majeraha hivyo anatakiwa kuwa nje ya uwanja ili
kutibu majeraha yake.
Michezo
mingine ambayo De Bruyne ataikosa ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya
UEFA dhidi ya Celtic unaotaraji kupigwa Jumatano na michezo miwili ya
Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Tottenham na Everton.
0 comments :
Post a Comment