Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amezungumzia tukio la kuteketea moto nyumba yake jioni
ya leo na kueleza kuwa licha ya moto huo kuunguza vitu mbalimbali, hakuna mtu yeyote aliyepata
madhara.
ya leo na kueleza kuwa licha ya moto huo kuunguza vitu mbalimbali, hakuna mtu yeyote aliyepata
madhara.
“Tumepata ajali kidogo. Nyumba yangu ninayoishi katika eneo la Kibingo, mji mdogo wa Mwandiga,
Kigoma imeteketea kwa moto jioni hii. Alhamdulillah, kuwa hakuna binaadam aliyeumia.”
Kigoma imeteketea kwa moto jioni hii. Alhamdulillah, kuwa hakuna binaadam aliyeumia.”
Zitto Kabwe ambaye yupo jijini Nairobi amelishukuru Jeshi la Zima Moto kwa namna lilivyoshughulika na ajali hiyo. Mbali na Polisi, Zitto ametoa shukrani zake kwa majirani wake
ambao kwa pamoja wamesaidia katika kuzima moto huo.
ambao kwa pamoja wamesaidia katika kuzima moto huo.
“Nawashukuru Jeshi la Zimamoto, majirani zangu pamoja na wananchi wenzangu kwa ushirikiano
walioutoa mpaka kuuzima moto husika.”
walioutoa mpaka kuuzima moto husika.”
Katika taarifa yake, Zitto amesema kwa sasa jeshi la polisi wanaendelea na uchunguzi kuweza
kubaini chazo cha moto huo na hivyo ni vyem wananchi wakawa watulivu ili polisi wafanya kazi
yao kwa utulivu.
kubaini chazo cha moto huo na hivyo ni vyem wananchi wakawa watulivu ili polisi wafanya kazi
yao kwa utulivu.

0 comments :
Post a Comment