Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha), Halima Mdee ataongoza mazishi ya aliyekuwa diwani wa viti maalumu Mbeya Mjini, Ester Mpwiniza yatakayofanyika kesho.
Taarifa ya Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Mbeya Mjini, Obadia Mwaipalu imesema mbunge huyo Ijumaa jioni alianguka nyumbani kwake na alipelekewa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya alikofariki dunia kutokana na shinikizo la damu.
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amesema Mpwiniza aliyewahi kuwa mwenyekiti wa Bawacha Wilaya ya Mbeya Mjini, alikuwa kiunganishi ndani na nje ya chama hicho, hivyo wameamua kumzika kesho Jumatatu.



0 comments :
Post a Comment