Baadhi ya wabunge na viongozi wa Chadema walioko nchini Kenya wamehudhuria ibada kumwombea Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.
Taarifa kutoka Nairobi zimesema ibada imefanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri.
Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa akizungumza na mwandishi wa Mwananchi, amesema hali ya Lissu inaendelea vizuri.
Pamoja naye, amesema wengine wanaohudhuria ibada hiyo ni Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche; Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita.
Mchungaji Msigwa amewashukuru wote walioonyesha mapenzi mema kwa Lissu na kwa Chadema.
Amesema waliofika Hospitali ya Nairobi kumjulia hali Lissu ni Jaji mstaafu, Mohamed Chande Othman; Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe.
Mchungaji Msigwa ametoa wito kwa Watanzania waendelee kumuombea na kutoa michango.
Lissu alishambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi Septemba 7 akiwa nyumbani kwake Area D mjini



0 comments :
Post a Comment