YANGA wametua mkoani Ruvuma kucheza na wenyeji Majimaji, wakiwa na dozi mkononi katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa Majimaji, mjini Songea.
Kikosi cha Yanga kilikuwa kimeweka kambi ya siku tatu mjini Njombe katika Hoteli ya Day To Day,
kiliondoka jana kwenda mkoani humo kikiwa na matumaini ya kuibuka na ushindi mnono dhidi ya
Majimaji.
Yanga, ambao ni mabingwa watetezi wa ligi hiyo, wataingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya
ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Njombe Mji, walioupata katika mchezo uliochezwa Jumapili iliyopita
kwenye Uwanja wa Sabasaba.
Ushindi huo unaonekana kuipa jeuri Yanga, lakini pia mazoezi ya nguvu waliyofanya wakiwa Njombe kabla ya kwenda kuwavaa wapinzani wao, Majimaji.
Kocha msaidizi wa Yanga Nsajigwa alisema malengo yao ni kuhakikisha wanaondoka na pointi tatu nyingine, kwani wamefanya maboresha katika kikosi chao kutokana na upungufu uliojitokeza mchezo uliopita.
Yanga walionekana kuanza msimu mpya vibaya, baada ya kufungwa kwa changamoto ya mikwaju ya
penalti 5-4, katika mchezo wa Ngao ya Jamii, baada ya kutoka sare ya kutofungana ndani ya dakika
90 kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Baadaye walitoka sare ya kufungana bao 1-1 na Lipuli, katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu Bara,
uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, kabla ya kusahihisha makosa yao na kuibuka na ushindi
katika mchezo uliofuata dhidi ya Njombe MjiFacebook