Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara, Yanga Sc imetupia lawama ubovu wa uwanja kuwa ndiyo sababu kubwa iliyowakosesa ushindi katika mchezo wa jana dhidi ya Majimaji FC.
Katika mchezo huo uliopigwa kunako dimba la Majimaji mjini Songea, Yanga ililazimika kusawazisha bao baada ya kutanguliwa na Majimaji na kufanya mchezo umalizike kwa sare ya bao 1-1.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo, kocha msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa amesema kutokana na ubovu huo, timu yake ilishindwa kuonesha kandanda la uhakika na ambalo lingewapa point tatu muhimu, badala yake wachezaji walikuwa wakicheza kwa shida na ‘butua butua’ za mara kwa mara.
Nsajigwa amesema uwanja huo ni mbovu na hauna hadhi ya kuchezewa mechi za ligi kuu na kuitaka TFF kulifanyia kazi suala hilo.



0 comments :
Post a Comment