Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba amesema kuwa bado anaamini Tanzania itapata katiba mpya ambayo itakuwa imebeba maoni ya wananchi.
Jaji Warioba amesema hayo katika mahojiano maalum na Azam TV nyumbani kwake jijini Dar es Salaam, na kusisitiza kuwa katiba hiyo ni lazima itazingatia maoni ya wananchi waliyoyatoa wakati wa mchakato aliouongoza yeye.
Amesema katiba hiyo ni muhimu ili kuweza kuondoa kasoro na dosari zinazojitokeza katika utendaji wa viongozi na kuweka sawa mipango yote ya maendeleo itakayofanywa na viongozi kwa mujibu wa katiba hiyo.
Waziri mkuu huyo wa zamani wa Tanzania amesema anaungana na wote wanaoshauri kuwa mambo yanayofanywa na rais Magufuli yainginzwe kwenye katiba lakini akawataka watambue kuwa tayari kuna maoni yaliyotolewa na wananchi, na hayo ndiyo yanayopaswa kuzingatiwa
0 comments :
Post a Comment