Baada ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kumtuhumu aliyekuwa msemaji wa klabu ya Yanga na mwandishi wa habari Jerry Murro kuwa Jeshi la polisi linatakiwa limchunguze kwa kusema alidai Mhe. Lema na Mbunge wa Arumeru, Joshua Nassari wanatakiwa wapotezwe. Hatimae Muro leo ameibuka na kujibu tuhuma hizo.
Muro akizungumza leo na waandishi wa habari amesema kuwa ni vyema mbunge huyo akajitafakari utendaji kazi wake jimboni kwake tangu kipindi cha nyuma alichokuwa akifuga rasta.
“Napenda kueleza kuwa walaka huo wenye kichwa cha habari wa kuhusu utoto wa Lema na Nassari niliuandika mimi na kikundi cha watu na kikundi cha vijana ambacho leo ntatoa ushahidi hapa waliamua kuchukua walaka huo na kuuhariri baadhi ya maneno na kuongeza baadhi ya vitu na kupunguza baadhi ya vitu sasa kwangu nimemshangaa Mhe. Lema na amenisikitisha sana kwasababu mbunge ambaye wananchi wamemuamini nilitegemea kwanza wao wangefanya uchunguzi kwa kuuliza huu walaka wa Jerry Muro ulikuwa na maneno haya? alihoji Muro.
“Na leo nataka Watanzania waone na waelewe nini maana ya tui la nazi na maziwa waone utofauti wa akili ndogo na akili kubwa katika haya mambo ambayo napenda wayajue, ukiona mbunge anaanza kuokota okota maneno na kufanya press na waandishi wa habari na kusema hiki kimesemwa na Jerry Murro pasipo kufanya utafiti pasipo kufuatilia hiki kitu ni cha Jerry Murro Mjue kabisa huyo sio kiongozi kwasababu wanaokota na kuokota huku kunapelekea kulipeleka Taifa kwenye mashaka,” amesema Jerry.
Hata hivyo Jerry Murro amemkumbusha mbunge Lema kutimiza wajibu wake kama mbunge wa Arusha ikiwa ni pamoja na kuwaletea maendelea kama afanyavyo Mkuu wa Arusha Mrisho Gambo na si kutembea na flash jijini Dar es salaam.
0 comments :
Post a Comment