Rais John Magufuli amesisitiza kuwa mbio za Mwenge wa Uhuru zitaendelea kuwepo nchini licha ya kupingwa na baadhi ya watu.
Rais Magufuli ametoa msimamo huo katika kilele cha mbio za Mwenge ambazo zimeambatana na kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Nyerere pamoja na siku ya vijana kitaifa, sherehe zikifanyika kitaifa mkoa wa mjini Magharibi visiwani Zanzibar.
Amesema kufuta mbio hizo kwa kisingizio cha gharama ni sawa na kufuta historia na alama ya nchi, hivyo katika kipindi chake cha uongozi hawezi kufanya jambo hilo.
“Mimi nawashangaa sana watu wanaotaka Mwenge ufutwe, sijui wanatoka sayari gani? Mimi siwezi kukubali Mwenge ufutwe, najua na Dkt. Shein hawezi kukubali mwenge ufutwe katika kipindi chake. Naomba muwazomee na muwasute hao wanaosema Mwenge ufutwe. Kufuta Mwenge wa Uhuru ni sawa na kufuta historia na alama za nchi yetu.” Amesema rais Magufuli.



0 comments :
Post a Comment