Watu wawili ambao walikuwa ni mume na mke wamepoteza maisha usiku wa kuamkia leo baada ya kuvamiwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi na kucharangwa mapanga katika kijiji cha Kasekese wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi.
Afisa mtendaji kata ya Kasekekese bwana Ramadhan Ibrahim amesema tukio hilo limetokea majira ya saa nne usiku ambapo watu hao walivamia nyumba ya marehemu.
ITV imefika katika hospitali ya manispaa ya Mpanda ambapo miili ya marehemu imehifadhiwa na kuzungumza na kaimu mganga mkuu wa hospitali hiyo Dokta Abel Nyika.
Kufuatia matukio hayo mkuu wa wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando amelaani vitendo hivyo na kuwataka wananchi kuwafichua wahalifu.



0 comments :
Post a Comment