Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Wlliam Lukuvi ameshiriki zoezi la kuvunja nyumba yake iliyokuwa imejengwa katika eneo la hifadhi ya barabara kuu iendayo katika hifadhi ya Ruaha.
Waziri huyo aliyetumia nguvu zake mwenyewe kuvunja nyumba hiyo iliyopo kijiji cha Mapogolo jimbo la Ismani mkoani Iringa, amesema lengo la hatua hiyo ni kupisha ujenzi wa barabara hiyo huku akiwataka wananchi wote ambao nyumba zao zimewekwa alama ya X kufuata nyayo zake kwa hiari badala ya kusubiri serikali kutumia nguvu.
Aidha waziri Lukuvi amezuia kuendelea kwa ujenzi wa shule mbili za sekondari ambao ulikuwa unaendelea katika kijiji cha Mauninga na kusema kuwa sera ya serikali hairuhusu kijiji kimoja kuwa na shule mbili huku akikemea ishara anazodai kuwa ni za ukabila kuwa chanzo cha ujenzi wa shule hizo katika kijiji kimoja.
Lukuvi anaendelea na mikutano na wananchi wa jimboni kwake kwa lengo la kupokea na kutatatua kero mbalimbali zinazowakabili wapiga kura