Vifaa kwa ajili ya mradi wa kupanua bandari ya Dar es Salaam vimewasili nchini tayari kwa kuanza kazi hiyo.
Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Fred Liundi amesema vifaa hivyo vilivyowasili nchini vitatumika kwaajili ya kupanua bandari hiyo itakayohudumu meli kubwa kutoka urefu wasasa wa mita 243 hadi kufikia mita 320.
Upanuzi wa bandari hiyo unafanywa na Kampuni ya China Harbour Enginering CO kutoka nchini China chini ya usimamizi, Anastazia Saled, ambapo mbali na kuongezwa kina cha bandari pia watajenga gati mpya kwa ajili ya kushusha magari.
Meneja huyo amewatoa wasiwasi watumiaji wa bandari hiyo kuwa ujenzi huo hautaadhiri utoaji wa huduma zozote zile bandarini hapo.