Mbunge wa Moshi vijijini na Mkurugenzi wa fedha na utawala wa chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) Anthony Komu amelituhumu gazeti la JAMVI LA HABARI kutumika na chama cha mapinduzi (CCM) kumchafua mwenyekiti wa Chadema kuhusu matumizi mabaya ya fedha za ruzuku za chama hicho.
Akizungumza leo makao makuu ya chama hicho Komu amesema gazeti hilo kwa wiki kadhaa sasa limekuwa likitoa tuhuma zisizo na ukweli juu ya matumizi mabaya ya fedha za ruzuku huku likimhusisha yeye na mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe.
“Hilo gazeti halijawahi hata kunihoji juu ya jambo hilo nikiwa kama Mkurugenzi wa fedha ila limekuwa mstari wa mbele katika kutoa tuhuma hizi ili kuwaaminisha wananchi kuwa Chadema si chama safi hii sio sawa kwa taaluma ya uandishi” Alisema Komu na kukitupia lawama chama cha mapinduzi kulifadhili gazeti hilo.
0 comments :
Post a Comment