Hii ni kwa mbinde Zanzibar Heroes kuukosa ubingwa wa CECAFA mwaka huu baada ya kufungwa kwa mikwaju ya penaiti 3-2 kwenye mchezo wa fainali uliochezwa leo.
Mchezo huo wa fainali uliowakutanisha wenyeji kenya dhidi ya Zanzibar umemalizika kwa Kenya kuibuka na Ushindi kwa njia ya matuta 3-2.
Awali mchezo huo ulichezwa kwa dakika 120, na kutoaka sare ya magaoli 2-2 na baadae ikaingia zamu ya matata.
Lakini upigianaji wa mikwaju ya penalti, Adeyum Seif aliyeingia dakika za nyongeza alikosa na mwisho Mohamed Issa 'Banka’ naye alikosa penalti zao zikipanguliwa na Wakenya wakafanikiwa kuibuka na ushindi huo wa mabao 3-2.
Licha ya kufungwa mchezo wa leo,Zanzibar, ilionyesha soka safi zaidi ya wenyeji Kenya na kufanikiwa kutoka nyuma mara mbili na kusawazisha mabao.
Zanzibar walionyesha soka la kitabuni tokea mwanzo na wachezaji wake walijituma kama ilivyokuwa tokea mwanzo katika michuano hiyo.
Mwisho wa yote ,Kenya ndiyo bingwa wa CECAFA 2017
0 comments :
Post a Comment