DED Morogoro Vijijini Kuchunguzwa

 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo ameagiza kufanyika uchunguzi wa haraka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya morogoro Vijijini  Sudi Mussa Mpiri kutokana na utendaji wake kutoridhisha ikiwemo kushindwa kutekeleza miradi ya maendeleo.
Pia  ameshindwa kutoa ufafanuzi wa fedha zilizopokelewa na Halmashauri hiyo kiasi cha sh.milioni 1.6 ya mapato ya ndani kutoka kampuni ya Dimond ambapo matumizi ya fedha hiyo zaidi ya asilimia 90 hayafahamiki kilichofanyika.
Kadhalika, Mkurugenzi huyo anadaiwa kuwa na mahusiano mabovu kati yake na watumishi wa Halmashauri hiyo.
Jafo alitoa agizo hilo akiwa Kijijini Mvuha kwenye makao makuu ya Halmashauri ya morogoro vijijini.
Kutokana na hali hiyo,Jafo ameagiza kitengo cha uchunguzi na ufuatiliaji kilichopo Ofisi ya Rais TAMISEMI kufika haraka kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini mwenendo wa mkurugenzi huyo kwa lengo la kuchukua hatua stahiki endapo itabainika kuna ufisadi na mapungufu ya kiuongozi kwa mkurugenzi huyo.
Katika hatua nyingine, Waziri Jafo hajarishishwa kabisa na miradi aliyo itembelea wilayani humo kutokana  na miradi hiyo imeonyesha wazi kwamba Halmashauri hiyo imefanywa kama shamba la bibi.
Jafo amewataka madiwani wa Halmashauri hiyo kufahamu kwamba wao wapo kwa niaba ya wananchi wanyonge hivyo wanapaswa kulinda na kusimamia  rasilimali za Halmashauri hiyo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment