Kiwango Cha Soka Tanzania Chazidi Kuporomoka


Tanzania imezidi kudidimia kwenye viwango vya soka duniani baada ya kushuka kwa nafasi 5 zaidi kwenye viwango vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kwa mwezi Novemba.

Kupitia taarifa iliyotolewa leo na FIFA, inaonyesha Tanzania inashika nafasi ya 147 kutoka  142 mwezi Oktoba, ikiwa imeporomoka kwa nafasi tano kutoka juu.

Kwa Uganda wa Afrika Mashariki na Kati, Uganda imeendelea kuongoza ikiwa inashika nafasi ya 75 duniani huku Senegal ikiwa inaongoza kwa Afrika nzima ikiwa inashika nafasi ya 23 kwenye viwango hivyo vya FIFA.
Kwa upande wa 10 bora, Ujerumani imeendelea kuongoza ikifuatiwa na Brazil, Ureno, Argentina, Ubelgiji, Hispania, Poland, Uswisi, Ufaransa na Chile.

Tanzania ilifanya vibaya kwenye michuano ya CECAFA nchini Kenya mapema mwezi huu pia kwa mwezi Novemba ilipata sare ya 1-1 dhidi ya Benin .- 
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment