Lema Hatakiwi Kuota Ndoto Bado Kijana Wazee Ndo Huota Ndoto ....Shahidi Mahakamani



MKUU wa upelelezi wilaya ya Arusha(OC-CID), Damas Masawe (44) amesema wazee pekee ndio wanaotakiwa kuota ndoto hivyo Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema hakustahili kuota ndoto dhidi ya Rais John Magufuli kwa kuwa bado ni kijana.

Ameyasema hayo leo mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Arusha ,Devotha Msofe wakati akitoa ushahidi wake kwenye kesi ya uchochezi namba 440/2016 inayomkabili Lema anayedaiwa kumdhalilisha Rais Magufuli.


Ameieleza mahakama kuwa kwa mujibu wa kitabu cha kitakatifu cha biblia imeandikwa wazee pekee ndio wataota ndoto hivyo kwa kuwa Lema hajafikisha umri wa miaka 60 hatakiwi kuota ndoto bali wazee wanaotakiwa, wapumzike ,watafakari na kuota ndoto.


Hata hivyo shahidi huyo alieleza mahakama hiyo kuwa ingawa yeye sio mtaalamu wa masuala ya imani lakini anaamini kuota ndoto sio kosa ila kosa ni kuadithia ndoto .
 

“Kuota ndoto sio kosa lakini kuadithia ndoto yako ni kosa hayo maneno laiti ningekutana naye uchagani kama kaka yake angeniambia wala nisingekuwa na shida lakini aliyatolea mkutanoni," alieleza Massawe.
 

NILIMTOLEA LEMA BASTOLA
 
Shahidi huyo ameieleza mahakama kuwa alilazimika kumtolea bastola mbunge Lema katika eneo la kambi ya Fisi juni 22, mwaka jana kwani alikuwa anajaribu kutoroka.


Massawe alida kwenye eneo hilo Lema alikuwa akihutubia mkutano wa hadhara huku akisisitiza hana ugomvi na Lema kwa kuwa hata watoto wa mbunge huyo wanampenda sana.


Awali ,Massawe akiongozwa na wakili wa serikali,Agnes Hyera kutoa ushahidi wake alidai kuwa kwenye mkutano huo wa Lema kulikuwa na watu 200.


Alidai kitendo cha Lema kumwita Rais Magufuli ana kiburi na kumtabiria kifo ni kuamsha chuki kwa wananchi waliomchagua na hakupendezwa na maneno hayo na hivyo aliamua kumchukulia hatua kwani kwa wakati huo alikuwa akikaimu nafasi ya mkuu wa polisi wilaya ya Arusha.(OCD).


Shauri hilo linalovuta hisia za wengi limeahirishwa mpaka Januari 22,mwakani litakaposikilizwa siku tatu mfululizo mpaka januari 24 ambapo upande wa mashtaka unatarajia kuendelea kuleta mashahidi wengine.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment